Ecclesiastes 3:19-21

19 aHatima ya mwanadamu ni kama ile ya wanyama; wote wana mwisho unaofanana: Jinsi anavyokufa mnyama, ndivyo anavyokufa mwanadamu. Wote wana pumzi inayofanana; mwanadamu hana cha zaidi kuliko mnyama. Kila kitu ni ubatili. 20 bWote huenda mahali panapofanana; wote hutoka mavumbini, mavumbini wote hurudi. 21 cNi nani ajuaye kama roho ya mtu huenda juu na roho ya mnyama hushuka chini ardhini?”

Copyright information for SwhKC